Tuesday, July 7, 2020

online-office-08

MAANA YA GRAPHICS NA MAARIFA YA KUZITENGENEZA/KUBUNI.


Pengine wewe ni miongoni mwa watu ambao hawafahamu 'graphics' ni nini. Kama unafahamu ni vizuri pia. Ila kama haufahamu naomba nitoe ufafanuzi wake kwa ufupi.

Picha za graphics ni picha zote ambazo zinabuniwa/kutengenezewa kwa kupambwa kwa maandishi yenye muonekano unaovutia pamoja na muunganiko wa picha nyingine nyingi/kadhaa zinazoweza kuwekwa kwenye picha moja—ili ionekane kuvutia zaidi.

Kuna mifano mingi sana ya picha za graphics. Baadhi ya mifano ya picha za aina hii ni: picha za matangazo mbalimbali ya biashara, kampuni au bidhaa fulani [zinazoweza kubandikwa kwenye makopo ya bidhaa husika, au kutembezwa na kuwekwa maeneo mbalimbali mtandaoni n.k.].

Mifano mingine ni picha zinazotumika kutangaza uwepo wa matukio mbalimbali kama vile tamasha, mikutano ya injili, uchaguzi na matukio mengine mengi. Vile vile graphics nyingine ni makava ya vitabu, business cards, picha za utambulisho kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, Whatsapp na YouTube [zilioongezewa madoido]. Lakini pia mifano mingine ni logo za tovuti au blogu, picha zilizo nje ya daftari tunazonunua kila siku [unaweza kuona zimepambwa kwa maandishi tofauti tofauti na picha ya mtu kuwekwa mahali hapo pia]. 

Iko mifano mingi sana. Hivi sasa, karibu kila mahali tunapokuwa kuna picha ya graphic karibu yetu. Hii ni kwa sababu picha hizi zinahitajika na kutumika maeneo mengi sana.

Picha zozote unazoziona zimetengenezwa kwa kuunganisha picha tofauti tofauti mahali pamoja na hata kuhusisha uwepo wa maandishi yenye muonekano unaovutia zaidi, hizo ndizo tunaziita graphics.

Hebu angalia, hata hizi picha tatu ulizoziona kwenye posti hii unayoisoma saa hizi ni picha za graphics.
Mifano mingine tumeiweka kwenye posti mojawapo ya blogu yetu, unaweza kuziangalia kwenye blogu hiyo kwa kufungua HAPA.

Sasa basi, unapoziona picha hizo tambua pia kuwa kuna namna ya kuzitengeneza. Kuna programu na Apps za aina tofauti tofauti zinazoweza kutumika kutengeneza picha hizi. Zipo Apps zinazofanya kazi vizuri kwenye kompyuta, lakini pia zipo zinazofanya kazi vizuri kwenye simujanja (smartphone) pia. Ikiwa unatamani kufahamu namna nzuri ya kuzitengeneza picha hizo, unahitaji tu kupata maarifa ya msingi na kuanza kuzitengeneza.

Nilisukumwa kuanza kuwaelekeza watu namna ya kubuni na kutengeneza picha hizi kwa sababu; Picha hizi zinahitajika sana, na idadi ya watu wanaotengeneza ni ndogo ukilinganisha na uhitaji wake. Ukipata maarifa haya muhimu utakuwa miongoni mwa watu wanaotengeneza picha hizi na kuziuza kwa watu wengi sana. 

Ili kuwafikia watu wengi zaidi, nimetoa pia na maelekezo ya namna ya kuwafikia watu wengi [wateja wa Graphics] waliopo mtandaoni—kwa urahisi sana kupitia Whatsapp.

Tumetumia audio za maelekezo ya hatua kwa hatua, tuna kitabu cha PDF (softcopy) cha maelekezo yote [kwa lugha ya kiswahili] na maelekezo ya moja kwa moja—kwenye kikundi chetu cha Whatsapp (Multifarious Knowledge House 04). 
BEI: Tsh 4500.
FOMATI: Audio & PDF.
IDADI YA KURASA [PDF]: 31.
UPATIKANAJI: WhatsApp [HAPA]/e-mail.

Ukiwa na shauku kubwa ya kujifunza maarifa ya msingi juu ya jambo hili, utaanza kutengeneza picha hizo ndani ya siku chache mno (siku 5 hadi 7). Hii ni kutokana na mpangilio wetu wa maelekezo haya na njia tunazotumia kukuelekeza. Karibu sana.


UNAHITAJI KUANZA KUJIFUNZA LEO? ILI NDANI YA SIKU CHACHE KWANZIA LEO UWE UMEANZA KUBUNI NA KUTENGENEZA GRAPHICS NZURI, KWA SMARTPHONE YAKO? NITAARIFU KWA KUJA INBOX KWANGU MOJA KWA MOJA—KWA KUFUNGUA HAPA.

Mifano mingine ya picha hizo iko HAPA.


MAARIFA HAYA YANAPATIKANA KWA NJIA YA WHATSAPP, KWA AUDIO ZILIZOREKODIWA TAYARI (mp3), KITABU CHENYE MAELEKEZO YOTE KWA MSAADA WA PICHA ZA HATUA ZOTE, NA MAELEKEZO YA MOJA KWA MOJA KWENYE KIKUNDI CHETU CHA WHATSAPP (MULTIFARIOUS KNOWLEDGE HOUSE 04) [HAPA].

KUJIUNGA NA KIKUNDI CHA WHATSAPP FUNGUA KWA KIGUSA HAPA [CLICK]

No comments:

Post a Comment